Sudan: Faru wa kipekee aliyekuwa amesalia duniani afa
Sudan, faru pekee wa kiume aina ya Northern White Rhino (Faru Weupe wa Kaskazini) aliyekuwa amesalia hai duniani, amekufa akiwa na miaka 45, shirika la Ol Pejeta limetangaza.
Faru huyo alikuwa akitibiwa kwa muda na matabibu katika shamba kubwa la uhifadhi wa wanyama la kituo hicho kwa muda kutokana na matatizo yaliyotokana na kuzeeka kwake.
Alikuwa na vidonda ambavyo vilikuwa vinakosa kupona kutokana na umri wake.
Shirika la Ol Pejeta limesema hali yake ilidhoofika sana katika kipindi cha saa 24 zilizopita.
"Hakuweza hata kusimama na alikuwa anateseka sana," Ol Pejeta wamesema kupitia taarifa.
Ripoti: Faru John alikufa kwa kukosa uangalizi wa karibu
"Matabibu wa wanyama kutoka kituo cha uhifadhi wa wanyama cha Dvur Kralove kutoka Jamhuri ya Czech, Ol Pejeta na Shirika la Wanyamapori kenya waliamua kukatisha uhai wake."
Sudan alikuwa maarufu sana duniani na alikuwa nembo ya kutetea juhudi za kupigana na ujangili na kuwaokoa wanyama walio katika hatari ya kuangamia.
Alinusurika kuuawa porini alipohamishiwa katika kituo cha kuhifadhi wanyama cha Dvur Kralove nchini Jamhuri ya Czech miaka ya 1970.
Mwaka 2009, alirejeshwa Afrika na kuanza kutunzwa katika kituo cha Ol Pejeta katika jimbo la Laikipia.
No comments:
Post a Comment
type your message here