Tuesday, 25 January 2022

 

Romario kuwania ugavana Rio de Janeiro, Brazil

 Seneta wa Brazil na mchezaji wa zamani Romario de Souza atawania wadhfa wa ugavana wa Rio de Janeiro mwezi Oktoba.

Jimbo hilo limekumbwa na ghasia na liko katika hatari ya kufilisika.

Mshindi huyo wa kombe la dunia la mwaka 1994 anajejulikana kama Romario anasema kuwa kampeni yake itaangazia kukabiliana na matatizo hayo.

Atakuwa mgombea wa chama cha mrengo wa kati cha Podemos. Amesifiwa kuwa seneta katika vita vyake dhidi ya ufisadi katika kandanda.

''Katika wakati huu wa ghasia, mabadiliko yanahitajika haraka. Rio ilikuwa na matatizo ya kiusalama, lakini sio kama sasa'' , mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 52 alisema siku ya Jumamosi akitangaza kuwania wadhfa huo.

Romario awali aliwania kuwa Meya wa Rio de Janeiro, lakini akajiondoa baadaye.Haki miliki ya picha

Romario awali aliwania kuwa Meya wa Rio de Janeiro, lakini akajiondoa baadaye
''Sina uzoefu wa kusimamia. Itakuwa kutokana na majaliwa ya Mungu , kwa mara ya kwanza kuonyesha kwamba nimekuwa na fursa kuonyesha kile nilichojifunza katika maisha yangu''.

Mchezaji huyo wa zamani wa Barcelona kwa sasa anachunguzwa kwa madai ya kuficha mali yake kwa lengo la kukwepa kulipa deni, kulingana na vyombo vya habari vya Brazil.
Amekana madai hayo.


No comments:

Post a Comment

type your message here

Top Post

BINAMU YAKE HALAND NI MOTO MWINGINE

Binamu yake Haland ni balaa lingine ambalo hukulijua. Unajua kafanya nini? Amecheza mechi 37... Ndani ya mechi 37 unajua kashind...