Friday, 7 October 2022

MBONGO ALIYEJIOLEA MZUNGU WA CALIFORNIA KIRAHISI KAMA KUMSUKUMA MLEVI, UTASHANGAA STORI HII

Mapya yaibuka ! Pichani mwanamama Deborah(60) ambaye ni afisa mstaafu wa jeshi la polisi nchini Marekani ameolewa na kijana huyo wa Kimasai toka Tanzania kwa jina la Saitoty Babu(30)

Akielezea, Deborah amesema mwaka 2017 aliingia Zanzibar yeye na binti yake kwa jina la Royce(30) ndipo wakiwa ufukweni wakaona vijana wawili wa kimasai mmojawapo akiwa ni huyo Saitoty. Kwasababu katika maisha yake hakuwahi kukutana na mtu toka jamii ya kimasai hasa aliyevaa kimasai, Debora aliomba kupiga nao picha kama ukumbusho, Saitoty akaomba atumiwe hiyo picha na ndipo akayapata mawasilianao ya Deborah wakawa wanawasiliana

Deborah alirudi kwao Califonia, Marekani lakini Saitoty akawa anawasiliana nae na kugusia kutaka kumuoa Deborah ambaye hakumpatiliza Saitoty hasa kwasababu wamepishana sana umri kwa miaka 30 na yeye binafsi Deborah japo alikuwa single lakini alikuwa anaishi kwa furaha. Haikuchukua miezi hata mitano Deborah alikuja kutalii tena Tanzania wakaonana tena. 

Siku moja Deborah akiwa anawasiliana na Saitoty kwa FaceTime, akamuonesha kwa watoto wake wengine wawili, wa kike Tiffany(32) na wa kiume Sherrick(27) ambao hawakuwa na hiana mama yao kuolewa na Saitoty sana sana walimuambia umri sio kigezo kama kakupenda na unaona mkiwa pamoja utakuwa na furaha basi sio mbaya kuolewa nae

Ambapo walifunga ndoa ya kimasai nchini Tanzania mwaka 2018 na mwaka huu 2022 ndio wamefunga ndoa ya kiserikali ila Deborah bado ana matumaini watafanya sherehe kubwa kwa mujibu wa mila za  kimasai ili familia zote mbili zijumuike. Pia amepewa jina la Kimasai anaitwa Nashipai na ameanza kutumia jina la mume wake huyo yaani Deborah Nashipai Babu

Baada ya kufunga ndoa, Debora amehamia Tanzania na wanaishi katika nyumba ya udongo(boma) na mume wake huyo maeneo ya Ubena. Deborah amesema maisha ya Marekani na Tanzania yanatofautiana sana ila bado anafurahia kuishi Tanzania licha ya kwamba kwasasa anapikia kwa kutumia kuni na maji walipo ni shida kidogo. Pia eneo wanaloishi kwasasa wanajenga Lodge

Changamoto ya penzi lao amesema ni watu baki au wananzengo kuwakalia kooni kwa kusema Saitoty amemuoa Deborah ili apate uhalali wa kwenda kuishi Marekani(green card) lakini Deborah amepangua kwa kusema mume wake huyo hata hana hamu kivile ya kwenda kuishi Marekani

Pia Debora amesema watu wengine wanamnanga kwa kumkejeli kuwa Saitoty ni mjukuu wake na wengine wakimwambia amemuasili(adopt) Saitoty. Ila amesema familia zao wote zimewapa baraka na kamwe hakuwahi kudhani angekuja kuolewa na mwanaume aliyempita sana umri ila wanapendana sana wote ni wacheshi na wote wapo romantic bila kusahau Saitoty hufanya chochote kile ili kumnunulia chocolate Deborah 

Saitoty ambaye anachunga mifugo amesema pia mke wake huyo ni mtu muhimu katika maisha yake kwani anamsapoti katika mambo mbalimbali 

📷: Deborah & Saitoty

No comments:

Post a Comment

type your message here

Top Post

BINAMU YAKE HALAND NI MOTO MWINGINE

Binamu yake Haland ni balaa lingine ambalo hukulijua. Unajua kafanya nini? Amecheza mechi 37... Ndani ya mechi 37 unajua kashind...