Habari (News)

MATOKEO KIDATO CHA NNE 2021/2022

BONYEZA HAPA KUYAONA MATOKEO YA KIDATYO CHA NNE







Sudan: Faru wa kipekee aliyekuwa amesalia duniani afa

Sudan, faru pekee wa kiume aina ya Northern White Rhino (Faru Weupe wa Kaskazini) aliyekuwa amesalia hai duniani, amekufa akiwa na miaka 45, shirika la Ol Pejeta limetangaza.
Faru huyo alikuwa akitibiwa kwa muda na matabibu katika shamba kubwa la uhifadhi wa wanyama la kituo hicho kwa muda kutokana na matatizo yaliyotokana na kuzeeka kwake.
Alikuwa na vidonda ambavyo vilikuwa vinakosa kupona kutokana na umri wake.
Shirika la Ol Pejeta limesema hali yake ilidhoofika sana katika kipindi cha saa 24 zilizopita.
"Hakuweza hata kusimama na alikuwa anateseka sana," Ol Pejeta wamesema kupitia taarifa.
Ripoti: Faru John alikufa kwa kukosa uangalizi wa karibu
"Matabibu wa wanyama kutoka kituo cha uhifadhi wa wanyama cha Dvur Kralove kutoka Jamhuri ya Czech, Ol Pejeta na Shirika la Wanyamapori kenya waliamua kukatisha uhai wake."
Sudan alikuwa maarufu sana duniani na alikuwa nembo ya kutetea juhudi za kupigana na ujangili na kuwaokoa wanyama walio katika hatari ya kuangamia.

Alinusurika kuuawa porini alipohamishiwa katika kituo cha kuhifadhi wanyama cha Dvur Kralove nchini Jamhuri ya Czech miaka ya 1970.
Mwaka 2009, alirejeshwa Afrika na kuanza kutunzwa katika kituo cha Ol Pejeta katika jimbo la Laikipia.




Makaburi yaliyo na 'ujumbe kutoka kuzimu' yagunduliwa Misri

Makaburi ya zamani ambayo yana majeneza kadha yaliyotengenezwa kwa mawe, na mkufu ulio na "ujumbe kutoka kuzimuni" vimegunduliwa nchini Misri.
Ugunduzi huo umefanywa Minya, kusini mwa Cairo. Makaburi yaliyogunduliwa ni ya zaidi ya miaka 2,000 iliyopita na shughuli ya ufukuzi inatarajiwa kuchukua miaka takriban mitano.

Waziri wa mambo ya kale Misri Khaled al-Enany amesema makaburi hayo yana majeneza 40, vito, vyungu na barakoa ya dhahabu.
Amesema kuna mashimo ya kuwekwa majeneza chini ya ardhi ambayo ni ya enzi za Mafirauni hadi enzi za Wagiriki mnamo mwaka 300BC hivi.
"Huu ni mwanzo tu wa 7ugunduzi huu mpya," aliwaambia waandishi wa habari.
"Karibuni tutaanza kuongeza kivutio kingine cha mambo ya kale Misri."



Tanzania na Kenya zinajitenga na Afrika? Ufa waibuka Bonde la Ufa na kuongeza uwezekano Afrika kugawanyika



Kuibuka kwa ufa mkubwa katika eneo la Suswa katika Bonde la Ufa kusini magharibi mwa Kenya kumezua wasiwasi kuhusu uthabiti wa eneo la Afrika Mashariki kijiolojia.
Wataalamu wanasema kutokea kwa ufa huo katika jimbo la Nakuru ni shughuli ya kijiolojia inayochukua muda mrefu ambayo imekuwa ikiendelea kwa muda.
Hilo limezua hatari ya kuanza kutokea tena kwa mitetemeko ya ardhi na milipuko ya volkano.
Wanajiolojia wanasema baada ya mamilioni ya miaka, bara la Afrika litapasuka na kuwa vipande viwili.

Sudan: Faru wa kipekee aliyekuwa amesalia duniani afa


Sehemu ya mpasuko itakuwa kwenye Bonde la Ufa jambo ambalo linazua uwezekano wa Kenya na Tanzania, pamoja na mataifa mengine ya Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika, kujitenga na bara la Afrika.
Mwanajiolojia David Adede ameambia BBC kwamba ufa huo ni sehemu ya kutengana kwa vipande viwili vikubwa vya bara Afrika ambako kutasababisha bara Afrika kutengana na kuwa mabara mawili.
Amesema shughuli hiyo imekuwa ikiendelea kwa muda lakini dalili zake zilikuwa zinafichwa na majivu ya volkano ambayo polepole yamekuwa yakiziba ufa kila unapotokea.
"Maji ya mvua yamesomba majivu hayo pamoja na mchanga na kuufanya ufa huo kuonekana zaidi," amesema.
Anasema vipande hivyo vimekuwa vikitengana "katika kasi ya sentimita mbili kila mwaka."
Kipande kilicho na sehemu kubwa ya bara hufahamika kama Kipande cha Nubia na kipande cha pili hufahamika kama Kipande cha Somalia.
Dkt James Hammond kutoka kwa Idara ya Sayansi na Uhandisi wa Dunia kutoka chuo cha Imperial College London alinukuliwa na jarida la mtandaoni la Mail & Guardian akisema: "Katika miaka milioni kadha ijayo, shughuli hii itakamilika na kuigawa Afrika mara mbili, na kuunda bahari mpya hapo katikati na bara jingine. Ukitumia jiografia ya sasa, bara hilo jipya litashirikisha Somalia, nusu ya Ethiopia, Kenya na Tanzania."

Baadhi ya wanajiolojia wanakadiria kwamba huenda mpasuko huu ukayabeba pia mataifa ya Uganda, Rwanda, Burundi na maeneo ya Malawi na Msumbiji.
Mwanajilojia Dereje Ayalew kutoka Chuo Kikuu cha Addis Ababa Ethiopia aliambia jarida hilo kwamba dalili za kutokea kwa bahari zimeanza kuonekana katika maeneo ya jangwani ya Ethiopia, eneo la Afar ambalo pia linahusisha baadhi ya maeneo ya Eritrea na Djibouti.



Mwaka 2005, alisema tayari nyufa nyingi zimeanza kutokea na ardhi imebonyea kwa hadi mira 100.
Ufa huo ulianza kuonekana wiki moja iliyopita baada ya mvua kubwa kunyesha na barabara ya Mai Mahiu kwenda Narok ikakatika eneo lenye ufa huo.
Awali, wengi waliamini ufa huo uliotokea Jumanne wiki iliyopita eneo la Karima ambalo linapatikana kilomita sita kutoka mji wa Mai Mahiu ulitokana na mvua kubwa.
Ufa huo uliokuwa umeikata barabara hiyo ulikuwa umeenea umbali wa mita 700.

Maafisa wa Mamlaka ya Taifa ya Barabara Kenya (KeNHA) wakishirikiana na mkandarasi kutoka China anayejenga reli ya kisasa, walifika eneo hilo na kuziba ufa.
Baada ya uchunguzi, ilibainika kwamba ulitokana na shughuli ya kijiolojia chini ya ardhi ambayo ilihusisha mvutano wa vipande vikubwa vya ardhi.
Siku chache baadaye Jumapili, ufa huo uliendelea kupanuka na kuathiri barabara hiyo tena jambo lililosababisha magari yenye kubeba mizigo mizito kutoweza kupita.
Aidha, ufa huo ulianza kuathiri nyumba za wakazi.
"Mkandarasi na kundi la wahandisi wamewekwa hapo kwa sasa na watasalia kuendelea kufuatilia yanayojiri kutokana na shughuli za kivolkano ambazo zilisababisha ufa huo," alisema naibu mkurugenzi wa mawasiliano wa KeNHA Charles Njogu baada ya ukarabati huo mara ya kwanza.
Bw Adede amesema hatua ya kuziba ufa huo kwa sasa itasaidia kwa muda mfupi tu.
Ufa huo umepitia katika baadhi ya nyumba na mashamba ya watu.

Mmoja wa walioathirika ni Eliud Njoroge, 77, ambaye ameambia BBC kwamba ameishi eneo hilo kwa zaidi ya miaka 20.
Anasema amelazimika kuibomoa nyumba yake na sasa analazimika kuishi kama 'mkimbizi' kwa jirani yake.

Mwandishi wa BBC aliyetembelea eneo hilo Gladys Njoroge anasema katika baadhi ya maeneo, ufa huo una upana wa mita 20 na kina cha hadi futi 50.

Wataalamu wametahadharisha kwamba nyufa zaidi zinaweza kuendelea kuonekana katika baadhi ya maeneo ya Bonde la Ufa.
Mwandishi wa BBC Ferdinand Omondi anasema viongozi wa eneo lililoathirika wamewahimiza wakazi wanaoishi karibu na maeneo yaliyotokea ufa huo kuhama, lakini baadhi kama Bw Njoroge hawawezi kuhamia mbali.








No comments:

Post a Comment

type your message here

Top Post

BINAMU YAKE HALAND NI MOTO MWINGINE

Binamu yake Haland ni balaa lingine ambalo hukulijua. Unajua kafanya nini? Amecheza mechi 37... Ndani ya mechi 37 unajua kashind...